Tuesday, August 23, 2016

UTEKELEZAJI WA AGIZO LA KUONDOA WATUMISHI WASIOSTAHILI KUWEPO KATIKA ORODHA YA MALIPO YA MSHAHARA SERIKALINI


MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO KAZI CHA WAZIRI KAIRUKI NA WATUMISHI WA UMMA MKOANI KAGERA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipitia hoja ya mmoja wa washiriki wa kikao kazi mkoani Kagera
Ufafanuzi wa hoja na kero mbalimbali mkoani Kagera ukitolewa na watalaam wakati wa kikao kazi
Bw. Welanika Sylivester akiwasilisha tatizo kuhusu kutopandishwa cheo kwa muda mrefu
Flora Kaigi akiwasilisha hoja kuhusu utaratibu wa kupandishwa daraja
Mmoja kati ya washiriki akiwasilisha hoja kuhusu walimu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiongea na Watumishi wa Umma mkoani Kagera kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi na wajibu wao wa kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje wakiwamo wananchi.

Monday, August 22, 2016

MHE. KAIRUKI ASIKILIZA KERO NA MAONI YA WATUMISHI WA UMMA MKOANI KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Mkoa wake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (kulia).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kushoto) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera  ikiwemo  kusafisha taarifa za watumishi mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (kulia) kuwasilisha taarifa ya Mkoa wake.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika Mkoani Kagera.

Mmoja wa watumishi wa  Umma  wa Mkoa wa Kagera akiwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika Mkoani Kagera.