Monday, June 23, 2014

BALOZI SEFUE AFUNGA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi, akiongea wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Meza kuu ikifuatilia burudani iliyotolewa na kikundi cha Machozi Theatre katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa taasisi mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipewa maelezo kuhusu maabara inayohamishika na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) Bw.Hiiti Sillo alipotembelea banda hilo kabla ya kufunga rasmi Maonyesho ya Wiki wa Utumishi wa Umma leo.


Kikundi cha Machozi Theartre kikitoa burudani.

No comments:

Post a Comment