Thursday, June 19, 2014

KONGAMANO LA MIAKA 50 YA MUUNGANO KATIKA UTUMISHI WA UMMA LAFUNGULIWA RASMI LEO

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI akifungua Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma 2014 katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mapema leo.

Sehemu ya Washiriki wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Mstaafu Bi.Ruth H. Mollel mapema leo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mapema leo. Kongamano hilo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2014
Sekretarieti ikichukua michango wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerer (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam mapema leo.

Katibu Mkuu mstaafu Bi. Ruth H. Mollel akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). Anayeonekana kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu, ambaye ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (wa tatu kutoka kulia) akiwa na wageni waalikwa wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma.Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Bw.Phillemon Luhanjo akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof.Sifuni Mchome.Kulia kwa mgeni Rasmi  ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu.Mgeni rasmi katika Kongamano la Miaka 50 ya Muungano ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bi.Hawa A. Ghasia (Mb) akiongea na vyombo vya habari baada ya ufunguzi katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa washiriki wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungan o katika Utumishi wa Umma akihojiwa na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment