Friday, October 17, 2014

KLABU YA MICHEZO YA UTUMISHI YAKABIDHI VIKOMBE KWA WAZIRI KOMBANI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuzipongeza timu zilizoshinda mashindano ya SHIMIWI yaliyomalizika mjini Morogoro hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo wa Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) (katikati) kuzungumza na watumishi katika hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda kwa kishindo katika Michezo ya SHIMIWI 2014.Kulia ni Mwenyekiti wa Michezo Utumishi Bw.Lumuli Mtaki.
Baadhi ya watumishi  wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda michezo ya SHIMIWI katika ukumbi wa Utumishi.
Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanaume kutoka Utumishi  Bw.Hassan Ligoneko akimkabidhi kombe Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akitoa mkono wa pongezi kwa Timu ya mpira wa pete ya Utumishi katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake.
Kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Elizabeth Fusi (kushoto) akimkabidhi kombe la mshindi wa kwanza mpira wa pete  Waziri wa Utumishi Mh.Celina O. Kombani (Mb) (katikati) katika hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda michezo ya SHIMIWI, iliyofanyika ukumbi wa Utumishi. Wengine wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) na Mwenyekiti wa Michezo wa Utumishi Bw.Lumuli Mtaki(kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (katikati) akitoa mkono wa pongezi kwa timu ya kamba ya Utumishi katika hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda michezo ya SHIMIWI, iliyofanyika ukumbi wa Utumishi. Wengine kwenye meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto), Mwenyekiti wa Michezo wa Utumishi Bw. Lumuli Mtaki (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (kulia) .
Baadhi ya watumishi  wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani)  wakati wa hafla fupi ya kuzipongeza timu za Utumishi zilizoshinda michezo ya SHIMIWI katika ukumbi wa Utumishi.

No comments:

Post a Comment