Saturday, October 11, 2014

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NDIO MABINGWA WA MPIRA WA PETE SHIMIWI 2014


Mabingwa wapya wa SHIMIWI 2014, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Afya na kunyakua kombe la SHIMIWI 2014 mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Hekaheka ya kuwania mpira baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za kijani) na Afya katika mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Afya aliyeruka juu akifanya jitihada za kuuzuia mpira ulioelekezwa golini  ili usilete madhara wakati wa mechi ya fainali ya SHIMIWI 2014 ulioikutanisha timu yake na Utumishi katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Mashabiki wa timu ya mpira wa pete ya Ofisi ya Rais,Utumishi wakiishangilia timu yao wakati wa fainali iliyoikutanisha timu yao na Afya katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.


Baadhi ya washabiki wa mchezo wa mpira wa pete wakishuhudia fainali kati ya Utumishi na Afya wakati wa mchezo uliozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.

No comments:

Post a Comment