Thursday, April 23, 2015

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YACHAGUA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2015

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakitoa salamu ya wafanyakazi wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015.

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili Bw. Methew Kirama mwenye Ipad (wa kwanza kushoto) akichukua matukio  wakati wa uchaguzi wa kumpata mfanyakazi bora wa ofisi ya Rais – Utumishi kwa mwaka 2015.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akimtangaza mfanyakazi bora wa ofisi wa mwaka 2015 mara baada ya uchaguzi kufanyika.

Mfanyakazi bora wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wa mwaka 2015 Bw. Francis Sangunaa (kulia) akiwashukuru watumishi baada ya kuchaguliwa

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akitoa maelekezo ya kumpata mfanyakazi bora wa ofisi kwa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment