Wednesday, June 17, 2015

BALOZI SEFUE AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akifungua Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Dr. Matern Lumbanga akitoa Mada kuu ya utangulizi katika Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti wa Kongamano, Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi, akitoa maelekezo kuhusu mada zilizowasilishwa wakati akiongoza kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma 2015.
Kaimu Katibu Mkuu-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue (hayupo pichani), kushoto ni Katibu Mstaafu Tume ya Utumishi Bi. Thecla Shangali, akifuatiwa na Katibu Mkuu Mstaafu-Ikulu Bi. Rose Lugembe.
Sehemu ya washiriki vijana "Young Professional" wakisikiliza maelekezo wakati wa Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma. 

No comments:

Post a Comment