Saturday, June 20, 2015

OFISI YA RAIS UTUMISHI YAMUAGA RASMI KATIBU MKUU MSTAAFU BW.GEORGE D. YAMBESI

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) iliyofanyika Leaders Club. Wengine ni Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi Bi.Celina O. Kombani (Mb) (wa pili kutoka kulia) na Mama Yambesi  (kushoto).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (hayupo pichani) iliyofanyika Leaders Club. Kushoto kwake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi.
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. George D. Yambesi (aliyesimama)  akizungumza katika hafla ya kuagwa iliyofanyika viwanja vya Leaders Club
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb)(kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. George D. Yambesi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika viwanja vya Leaders Club. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (wa pili kutoka kulia) akipokea kombe la mshindi wa kwanza wa mpira wa pete la mashindano ya Mei Mosi 2015 kutoka kwa Kapteni wa Timu ya Netiboli ya utumishi Bi. Elizabeth Fusi katika viwanja vya Leaders Club. Wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Mama Yambesi (kushoto).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb) (wa pili kutoka kulia) akionyesha Tuzo ya Ununuzi Bora wa Umma  ya Ofisi ya Rais - Utumishi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) hivi karibuni baada ya kushinda.Wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Mama Yambesi (kushoto).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika hafla ya kumuaga Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi iliyofanyika Leaders Club.No comments:

Post a Comment