Thursday, October 1, 2015

MWILI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS-UTUMISHI MHE. CELINA O. KOMBANI (MB) WAPUMZISHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE.......

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akisoma wasifu wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa Ibada ya kuuga mwili wake iliyofanyika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma (kulia) ukiwa mbele ya wafiwa wakati wa Ibada ya kuuga iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Baadhi ya waombolezaji wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. 

Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. Ghalib Bilali (wa tano kutoka kulia) akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (wa nne kutoka kulia) wakishiriki ibada ya kuuaga Mwili wa marehemu Mhe. Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. 

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu Celina O. Kombani  (Mb) Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment