Monday, January 25, 2016

Serikali yafungua rasmi mafunzo ya ukusanyaji Taarifa za Tathmini ya Kazi

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kufungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akifungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

Timu ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi baada ya kufungua mafunzo kwa timu hiyo kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. Waliokaa kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba. 

No comments:

Post a Comment