Tuesday, February 23, 2016

Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaendelea na Vikao kazi kwa Njia ya Video (Video Conference)

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (picha ndogo kulia) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video kilichohusisha Ofisi ya Rais-Utumishi,Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda, Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na ofisi za Sekretarieti za mikoa ya Iringa, Pwani, Mtwara, Dar es Salaam, Kagera,Kigoma.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Sakina Mwinyimkuu (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu Uimarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini kwenye kikao kazi kwa njia ya video kilichofanyika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).

Washiriki wa kikao kazi kwa njia ya video wakimsikiliza mtoa mada.

No comments:

Post a Comment