Thursday, June 23, 2016

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 7 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan, Bi.Yuka ITO, akielezea namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo. 
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika  ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Yuka ITO aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba ( wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na  wawakilishi kutoka JICA.

No comments:

Post a Comment