Thursday, July 14, 2016

UTUMISHI YATOA UFAFANUZI KUHUSU MASUALA MBALIMBALI YA KIUTUMISHI KATIKA KIPINDI CHA MORNING TRUMPET KINACHORUSHWA NA AZAM TV

Mtangazaji wa Kipindi cha “Morning Trumpet” kinachorushwa na AZAM TV,  Bw. Faraja Sendegeya (kushoto)  akifanya mahojiano na Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma , Bw. Mathias Kabunduguru – Mkurugenzi wa Undelezaji Sera (katikati) na Bw. Nyakimura Muhoji - Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma.  Kipindi hicho kililenga kutoa elimu kwa umma juu ya masuala mbalimbali ya kiutumishi na kilirushwa mapema leo.

Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Kipindi cha “Morning Trumpet “ kinachorushwa na AZAM TV. Katikati ni Mkurugenzi wa Undelezaji Sera wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathias Kabunduguru na kushoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Faraja Sendegeya. 

Mkurugenzi wa Undelezaji Sera wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathias Kabunduguru akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Kipindi cha “Morning Trumpet “kinachorushwa na AZAM TV.  Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Nyakimura Muhoji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kushoto ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bw. Faraja Sendegeya.

No comments:

Post a Comment