Thursday, August 4, 2016

BALOZI WA JAMHURI YA KOREA AMTEMBELEA MHE. KAIRUKI KUZUNGUMZIA MASUALA MBALIMBALI YA MAENDELEO NCHINI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Jamhuri ya Korea uliomtembelea ofisini kwake leo kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo nchini. Wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe. Song, Geum-young, Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Afrika wa Wakala ya Mtandao na Usalama ya Korea, Dkt. Tae Seung Lee na Katikati ni Afisa Mambo ya Nje, Bw.Abdallah Kilungu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe. Song, Geum-young (wa pili kushoto) alipomtembelea Waziri kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo nchini akiwa na Mkurugenzi wa Afrika wa Wakala ya Mtandao na Usalama ya Korea Dkt. Tae Seung Lee (wa kwanza kushoto) na katikati ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Abdallah Kilungu.

No comments:

Post a Comment