Wednesday, August 10, 2016

WASIMAMIZI WA MIRADI YA TEHAMA SERIKALINI WAPEWA MAFUNZO

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Arnold Mathoyo akieleza utaratibu wa mafunzo ya TEHAMA kwa washiriki wanaosimamia miradi ya TEHAMA chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

Washiriki wa mafunzo kuhusu TEHAMA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani).

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa wataalam wa TEHAMA wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawii akifungua mafunzo kwa wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.
No comments:

Post a Comment