Sunday, September 25, 2016

LIJUE GAZETI LA SERIKALI

GAZETI LA SERIKALI-sehemu iliyopita tuliona matumizi ya taarifa zinazochapishwa katika gazeti la serikali ikiwamo kufuatilia masuala mbalimbali ya kisheria, na aina ya taarifa hizo.
Leo tunaangalia lugha inayotumika katika Gazeti la Serikali, bila shaka umewahi kujiuliza kuhusu jambo hili. Lugha inayotumika katika taarifa za Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kanuni C. {2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la 2009 na Establishment Circular letter No. 7 ya mwaka 1970, taarifa zote zinatakiwa kuwa katika lugha ya Kiswahili isipokuwa taarifa zinazohusu matangazo ya Kisheria, kwa maana ya Miswada ya Bunge na matangazo ya Serikali, Government Notice, ambayo hutangazwa kwa lugha ya Kiingereza.

https://www.facebook.com/utumishiweek

Gazeti la Serikali hupatikana wapi?, itaendelea..

1 comment:

  1. Kuna gazeti la serikali ambalo limo katika website hii la 17 Januari 2014. Uki=download unarudi ujumbe "error while downloading file" aje?

    ReplyDelete