Tuesday, September 13, 2016

KATIBU MKUU,OFISI YA RAIS-UTUMISHI DKT. LAUREAN NDUMBARO AZINDUA MASHINDANO YA SHIMIWI YA MWAKA 2016 KWA NIABA YA KATIBU MKUU BALOZI MHA. JOHN W.H. KIJAZI WAKATI WA BONANZA LA WATUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akisoma risala kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mha. John W. H. Kijazi wakati wa Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akimkabidhi Kombe la mshindi wa kwanza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Theresia Mmbando baada ya watumishi wa ofisi yake kuhudhuria kwa wingi zaidi ya taasisi zote katika Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa Bonanza la uzinduzi wa Mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka 2016 wakipita katika barabara ya Mandera kuelekea Uwanja wa Uhuru ikiwa ni sehemu ya bonanza hilo.
No comments:

Post a Comment