Tuesday, September 6, 2016

WADAU WAJADILI MPANGO KAZI WA KUENDESHA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OGP) WA AWAMU YA TATU


Baadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu  wakimsikiliza  Katibu Mkuu Ikulu  Bw. Peter Ilomo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akichangia mada katika mkutano wa wadau wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP)  wa Awamu ya Tatu,  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam.  Bw. Ilomo alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi (katikati) akifafanua hoja kuhusu Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi akisisitiza jambo kuhusu Mpango Kazi  wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


No comments:

Post a Comment