Thursday, November 10, 2016

SERIKALI YAPOKEA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Naibu Balozi Msafiri Marwa akizungumza na Wataalam wa Kujitolea kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao ambao watafanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini kwenye sekta za Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii, hafla iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi.

Mratibu wa Wataalam wa Kujitolea kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), Bw. Mada Hideki akifafanua jambo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Naibu Balozi Msafiri Marwa (hayupo pichani) katika hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam saba wa kujitolea iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Naibu Balozi Msafiri Marwa akimsikiliza Mratibu wa Wataalam wa Kujitolea kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), Bw. Mada Hideki katika hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam saba wa kujitolea iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Naibu Balozi Msafiri Marwa akiagana na Wataalam wa Kujitolea kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao ambao watafanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini kwenye sekta za Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii.


No comments:

Post a Comment