Tuesday, December 13, 2016

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHITIMISHA WIKI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAADILI KITAIFA NA HAKI ZA BINADAMU NCHINI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na Idara ya Ukuzaji Maadili ya Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Dini wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa nchini na wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipokuwa akifunga rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza wakati wa kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihitimisha kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua Makati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu siku ya kilele cha Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili Kitaifa na Haki za Binadamu iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment