Friday, March 3, 2017

UTUMISHI YAKABIDHIWA MAGARI MAWILI NA JICA

Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), Bw. Toshio Nagase (kulia) katika hafla fupi ya kupokea magari mawili (2) yaliyotolewa na JICA leo katika ukumbi wa JICA. 
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA, Bw. Toshio Nagase (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari kwa Ofisi ya Rais -Utumishi katika ukumbi wa JICA mapema leo. Wa kwanza kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Mahusiano kwa Umma wa JICA, Bw. Raymond Msoffe.


Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wa Ofisi ya Rais–Utumishi, Bw. Peter Mabale akihakiki vibali vya mojawapo ya gari lililokabidhiwa kwa Ofisi ya Rais - Utumishi kutoka JICA.

Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) akipokea funguo za magari kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi Dr. Laurean Ndumbaro kutoka kwa Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase (kushoto) katika ofisi za JICA mapema leo. 
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais- Utumishi na JICA mara baada ya hafla ya makabidhiano ya magari katika ofisi za JICA jijini Dar es salaam.

Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase (kushoto) akiangalia usajili wa mojawapo ya gari akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba mapema leo.


Mojawapo ya gari lililokabidhiwa leo kwa Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

No comments:

Post a Comment