Friday, July 21, 2017

TAREHE 31 OKTOBA, 2017 KUWA MWISHO WA KUDAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KUPITIA FOMU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa kada mbalimbali wa Tarafa ya Ukonga alipofanya ziara ya kikazi  ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. 

Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Furaha, Bw. Daniel Song’oa akiwasilisha malalamiko yake wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua hoja mbalimbali alizopokea kutoka kwa watumishi wa umma wa Halmashauri Manispaa ya Ilala – Tarafa ya Ukonga (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Msongela Palela na kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo.


No comments:

Post a Comment