Tuesday, July 11, 2017

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA WATUMISHI WA UMMA HALMASHAURI YA WILAYA YA TEMEKE KATA YA MBAGALA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke alipofanya ziara katika tarafa hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba. 
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bibi. Theresia Mmbando akizungumza na watumishi wa umma Tarafa ya Mbagala kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki (kulia) leo wakati wa ziara yake katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.Afisa Elimu Kata ya Mbagala Kuu Bibi. Mindi Kuchilingulo akichangia mada wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.


Katibu Tawala Wilaya ya Temeke Bw. Hashim Komba akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhe. Waziri Angellah Kairuki. 
Mkurugenzi Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw. Issa Ng’imba akielezea shughuli zinazofanywa na idara yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya watumishi wa umma kutoka tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke wakifuatilia hoja zilizokua zikiendelea wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah J. Kairuki kusikiliza kero za watumishi wa umma leo katika tarafa ya Mbagala Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment