Sunday, August 13, 2017

Ofisi ya Rais-UTUMISHI yawakaribisha Wataalam watano wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliokuja kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani (hawapo pichani) waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini 
baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI.Wengine ni wafanyakazi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Thursday, August 3, 2017

KATIBU MKUU UTUMISHI AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA MADEREVA WA SERIKALI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro  (mwenye tai) katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali (CMSP) mara baada ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ofisini kwake mjini Dodoma leo.


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MASAA YA KUNYONYESHA KWA MAMA ALIYEAJIRIWAMiundo ya Utumishi wa Umma

Tembelea link ifuatayo kusoma Waraka Na.1 wa mwaka 2004 kuhusu Utekelezaji wa Miundo ya Utumishi wa Umma;
http://www.utumishi.go.tz/utumishiweb/index.php?option=com_phocadownload&view=file&id=398:waraka-wa-utumishi-na-1-wa-2004-kuhusu-utekelezaji-wa-miundo-ya-utumishi&Itemid=180&start=20&lang=en

Miundo ya UTUMISHI

"Watumishi wa Umma ambao Miundo yao ya Maendeleo ya Utumishi iliwataka kuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha Nne wakati wanaajiriwa, na ambao hawajawasilisha vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania mishahara yao isimamishwe kuanzia mwezi Julai, 2017 hadi watakapowasilisha vyeti hivyo kwa ajili ya kuhakikiwa"
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Julai 13/2017